Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, utawala wa Kizayuni uliendelea na mashambulizi yake dhidi ya maeneo ya kusini mwa Lebanon wakati huo huo na safari ya Papa Leon wa Kumi na Nne kwenda Lebanon. Katika mashambulizi hayo, jeshi la utawala wa Kizayuni lilirusha mabomu kuelekea miji na vijiji kadhaa, na pia kushambulia baadhi ya maeneo kwa mashambulizi ya moja kwa moja ya mizinga.
Kituo cha kijeshi cha Kizayuni kinachojulikana kwa jina la “Roisat al-‘Alam” kilishambulia mara kadhaa pembezoni mwa mji wa Kafr Shuba kwa risasi za kivita jioni ya Jumapili; aidha, kikosi cha Kizayuni kilichokuwa kimejikita katika eneo la “al-Jirdah” kilifyatua risasi mfululizo kuelekea maeneo ya kandokando ya mji wa al-Dhahira.
Vilevile, ndege isiyo na rubani ya Israel ilirusha bomu la sauti kuelekea mji wa Maroun al-Ras, na ndege nyingine zisizo na rubani pia zilirusha mabomu ya sauti karibu na wavuvi wa samaki katika eneo la Ras al-Naqoura.
Katika shambulio jingine, ndege isiyo na rubani ya Kizayuni ilishambulia kifaa cha kuchimbia (mtambo wa kuchimba) katika kitongoji cha al-Wasatani kilichopo ndani ya mji wa Shabaa.
Wakati huohuo, jeshi la utawala wa Kizayuni kwa kufyatua risasi kuelekea eneo la Wadi Madhlim lililoko karibu na mji wa Beit Lif, liliuchochea zaidi mvutano wa hali ya usalama, na kwa wakati mmoja, kuruka kwa mfululizo ndege za upelelezi na ndege zisizo na rubani za Israel kulishuhudiwa katika anga ya eneo hilo.
Pia, makombora ya moto yalirushwa kuelekea eneo lililopo kati ya mji wa Beit Lif na mji wa Ramia. Katika kuendeleza mashambulizi haya, wanajeshi wa Kizayuni walirusha makombora kuelekea upande wa kusini-magharibi wa mji wa Yaroun, na hapo awali pia walikuwa wamefanya oparesheni za upekuzi na kufyatua risasi hewani katika eneo la linalozunguka mji wa Aitaroun.
Maoni yako